[kictanet] Day 3 of 10: How to Develop Skilled Human Capital

Wangari Kabiru wangarikabiru at yahoo.co.uk
Sun Jun 26 10:37:50 EAT 2016


Baraka tele za Jumapili!

Katika kuchangia mada hii ambayo yahusiana na watu, ujuzi na hali ya kikazi kila siku, ni muhimu kuangalia mswada wa lugha.

Tukianza na nakala hii iliyotolewa na Ofisi ya Serikali ili iwe ya mazungumzo na nakala zinginezo, ili kuzungumzia jamii kubwa ya wakenya yafaa kuwa na nakala kwa lugha ya Kiswahili ambayo ni lugha ya taifa. Je, ipo?
La sivyo, washirika ni wale wale wanaoelewa lugha ya kimombo. Zaidi ya hapo na muhimu zaidi, yatenga jamii kubwa sana ya wahusika.

Tukisonga mbele katika mswada wa "How to Develop Skilled Human Capital", tukilinganisha na lugha, inamaana yakwamba maendeleo yatakayotokana na uchambuzi huu yafaa kuikuza, kueneza na kuendeleza lugha ya Kiswahili katika jamii na nchi kwa ujumla. 

La sivyo, ni kueneza ukoloni mamboleo kwa utani - chini ya maji. Kwani lugha na matumizi yake katika mambo ya kila siku ndiyo huunganisha na katika hayo kuikuza lugha.

Hapa pia tukikumbuka yakwamba lugha ya Kiswahili ni lugha rasmi katika bara la Afrika.

Nawatakia majadiliano mema pia katika wiki ijayo!

Siku njema yenye baraka tele.

Mi mimi wako/ Wangari


On Jun 24, 2016 08:18, Walubengo J via kictanet <kictanet at lists.kictanet.or.ke> wrote:
>
> Listers,
>
> Plse feel free to contribute on previous threads as long as you pick the corresponding title.  Also remember, for those wishing to directly edit the Draft ICT policy, visit Jadili platform, register and post.
>
> So onto todays theme:
> How to Develop Skilled Human Capital 
>
> *ICT integration in primary, secondary, tertiary levels,
> *Specialized Skills (Software /Engineering)
> *Research & Development Capacity
> *eLiteracy for citizens/public 
>
> The Background:
> The Digital Literacy Program aka the Laptop project is ongoing and we probably have  to wait another 18-20yrs years to  see its impact (when today’s std 1s hit the market).  But meanwhile, we need skilled human capital to help move us from a net consumer of electronic goods and services into a net producer of the same.
>
> Our R&D output in general is quite low (Global Innovation Index 2015) despite the fact that we are leader at a regional level.  What should the Policy capture  to ensure Kenya churns out a constant supply of  highly skilled manpower necessary to drive the digital society.
>
> Send in your ideas, comments, strategies, etc. 
>
> 1Day as usual for the topic.
>
> walu.
>  
-------------- next part --------------
An HTML attachment was scrubbed...
URL: <https://lists.kictanet.or.ke/pipermail/kictanet/attachments/20160626/b22cc606/attachment.htm>


More information about the KICTANet mailing list